Call for Interview 13-09-2025: Walioitwa Kwenye Usaili. Tazama orodha ya majina yaliyochaguliwa kwa usaili tarehe 13 Septemba 2025.
Wasailiwa wote wanapaswa kusoma maelekezo yafuatayo kabla ya kuwasili lwenye vituo vya usaili.
1. Usaili utafanyika kuanzia tarehe kama ilivyooneshwa kwenye tangazo hili muda na sehemu ambapo usaili utafanyika umeainishwa kwa kila Kada.
2. Kila msailiwa anatakiwa kufika kwenye eneo la usaili akiwa amevaa Barakoa (Mask)
3. Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi;
4. Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:- Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho cha Mpiga kura,Kitambulisho cha kazi,Kitambulisho cha Uraia au Hati ya kusafiria.
5. Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti cha kuzaliwa,kidato cha IV, VI, Stashahada,Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea kutegemeana na sifa za Mwombaji.
6. Wasailiwa watakaowasilisha Testimonials, Provisional Results, Statement of results, hatiza matokeo za kidato cha IV na VI (form V and form VI results slips) HAVITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI.
7. Kila msailiwa atajigharamia kwa Chakula, Usafiri na Malazi.
8. Kila Msailiwa azingatie tarehe, muda na mahali alipopangiwa kufanyia usaili.
9. Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (kama TCU, NACTE au NECTA)
10. Waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakukidhi vigezo. Hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa na kuzingatia mahitaji ya tangazo husika.
11. Kwa kada ambazo wanatakiwa kusajiliwa na Bodi zao za Kitaaluma wanapaswa kuja na vyeti vyao Halisi vya Usajili pamoja na Leseni za kufanyia kazi.
12. Wasailiwa wote walioitwa kwenye usaili wahakikishe wanaingia kwenye akaunti