Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga anapenda kuwatangazia watanzania wote wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi ya kazi ya Msaidizi wa Kumbukumbu Daraja La II (Nafasi 04) na Dereva Daraja la II (Nafasi 10) za ajira ya masharti ya kudumu, Baada ya kupata idhini ya kutangaza nafasi za ajira kwa Kibali kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kupitia barua yenye Kumb. Na. FA. 97/288/01/A/25 ya tarehe 29 Aprili, 2025.
Hivyo anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa za kujaza nafasi zifuatazo;-
1. MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA II NAFASI (4)
SIFA ZA MWOMBAJI: Mwombaji awe na Cheti cha Kidato cha Nne (IV) au Kidato cha Sita (VI) aliyehitimu Stashahada au NTA level 6 katika fani ya Utunzaji wa Kumbukumbu, kutoka Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali, na mwenye ujuzi wa Kompyuta.
NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali na ajira ya kudumu (TGS, C)
2. DEREVA DARAJA LA II (NAFASI 10)
SIFA ZA KUAJIRIWA Kuajiriwa wenye cheti cha Kidato cha Nne (Form IV) na Leseni ya Daraja E au C ya uendeshaji magari ambayo wamefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja (1) bila kusababisha ajali pamoja na vyeti vya mafunzo vilivyowapatia sifa ya kupata madaraja husika. Wawe wamehudhuria mafunzo ya msingi ya Uendeshaji magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na Chuo cha VETA au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.
NGAZI YA MSHAHARA Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali na Ajira ya Kudumu (TGS, B+ 638.)
Masharti ya Jumla kwa Waombaji wa Kazi Tanzania
Unapojipanga kuomba ajira serikalini au taasisi mbalimbali hapa Tanzania, ni muhimu kujua masharti ya jumla ya waombaji wa kazi. Mara nyingi waombaji hukataliwa kutokana na kutozingatia maelekezo rahisi yanayotolewa kwenye tangazo la kazi. Makala hii itakuongoza kupitia masharti muhimu ambayo kila mwombaji anatakiwa kuyazingatia.
1. Uraia na Umri wa Mwombaji
Waombaji wote wanapaswa kuwa Raia wa Tanzania wenye umri kuanzia miaka 18 hadi 45. Hata hivyo, kwa waombaji walioko kazini Serikalini, ukomo wa umri unaweza ukawa tofauti kulingana na nafasi husika.
2. Maelezo Binafsi (CV)
Mwombaji anatakiwa kuwasilisha Curriculum Vitae (CV) yenye maelezo ya kutosha. CV hiyo inapaswa kujumuisha:
-
Anuani sahihi na namba za simu za kuaminika
-
Majina ya wadhamini watatu (Referees) wenye sifa na uaminifu
Hii husaidia waajiri kupata picha kamili ya uwezo na historia ya kitaaluma ya mwombaji.
3. Vyeti na Hati Muhimu
Waombaji wote wanatakiwa kuambatanisha:
-
Nakala za vyeti vya Kidato cha Nne au Sita
-
Vyeti vya kitaaluma
-
Cheti cha kuzaliwa
Muhimu: Vyeti vya aina ya Result Slip, Statement of Results, Provisional Results au Transcripts HAVITAKUBALIKA kama mbadala wa vyeti rasmi.
4. Waombaji Waliosoma Nje ya Nchi (Sekondari)
Ikiwa umehitimu elimu ya sekondari nje ya Tanzania (Kidato cha Nne au Sita), ni lazima uwasilishe uthibitisho kutoka Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA).
5. Waombaji Waliosoma Vyuo vya Nje
Kwa wale waliomaliza masomo ya juu nje ya nchi, ni lazima uwasilishe uthibitisho kutoka Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU). Hii ni hatua ya kuhakikisha sifa zako za kitaaluma zinatambulika rasmi nchini.
Unakumbushwa kuambatanisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu. Barua zote za maombi ziandikwe kwa
Mkurugenzi Mtendaji,
Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga,
S.L.P 113,
Iselamagazi- Shinyanga.
Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa 'Recruitment Portal').