Makala ya Nafasi Mpya ya Kazi Zilizotangazwa kutoka Zanzibar kupitia tovuti ya zanajira.go.tz. Nafasi iliyotangazwa ni Mkaguzi wa Hesabu Daraja la II-UNGUJA, Kwa wote wenye Taaluma hiyo wanapaswa kufanya maombi au kutuma maombi kabla ya tarehe 13 Septemba 2025 kupitia website ya ZanAjira.
Muda wa Kutuma Maombi: 29-08-2025 To 13-09-2025
Haya ndiyo majukumu ya Mkaguzi wa Hesabu Daraja la II-UNGUJA - 1 POST
1. Kufanya ukaguzi wa hesabu za Serikali kwa Wizara, Mashirika, Wakala, Mamlaka pamoja na Miradi ya Maendeleo.
2. Kufanya utekelezaji wa mpango kazi wa ukaguzi wa kila mwaka.
3. Kufanya ufuatiliaji wa hoja za ukaguzi zinazotolewa baada ya ukaguzi kukamilika.
4. Kuandaa ripoti za ukaguzi kwa wakati.
5. Kutunza na kuweka kumbukumbu mbalimbali za kazi za ukaguzi katika eneo lake la kazi.
6. Kufanya kazi nyingine zozote zinazohusiana na kada yake atakazopangiwa na mkuu wake.