WhatsApp Group Join Now

Tangazo la Kazi Bunda 04-09-2025

 

Tangazo la Kazi Bunda 04-09-2025

Tangazo la Kazi Bunda 04-09-2025

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri (W) ya Bunda anawatangazia Watanzania wenye  sifa kuomba nafasi za kazi kumi na Saba (17) katika Halmashauri hii baada ya kupata kibali kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa mchanganuo ufuatao:

1.MWANDISHI WAENDESHA OFISI DARAJA LA II - (NAFASI 1)

Sifa ya Muombaji Mwandishi Waendesha Ofisi

Awe amehitimu Elimu ya Kidato cha Nne (Form IV) au Kidato cha Sita (Form VI),  aliyefuzu mafunzo ya Stashahada ya uhazili (NTA LEVEL 6), Awe amefaulu somo  la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 100 kwa dakika moja. Awe  amepata mafunzo ya Komputa kutoka chuo chochote kinachotambulika na Serikali na kupata cheti katika “Program za Windows, Microsoft Office, Internet, E-mail na Publisher”.

2. MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA II (RECORDS MANAGEMENT ASSISTANT II) - (NAFASI 04)

Sifa ya Muombaji Msaidizi Wa Kumbukumbu 

Awe amehitimu elimu ya Kidato cha Nne (IV) au Sita (VI) mwenye Stashahada (NTA Level 6) katika fani ya Utunzaji wa Kumbukumbu kutoka Vyuo vinavyotambulika na Serikali.

3. MSAIDIZI MAENDELEO YA JAMII DARAJA LA II - (NAFASI 02)

Sifa ya Muombaji Msaidizi Maendeleoya Jamii

Awe amehitimu elimu ya Kidato cha Nne (IV) au Sita (VI), awe mwenye Astashahada (Certificate) ya Maendeleo ya Jamii kutoka vyuo vya Maendeleo ya Jamii au Vyuo vingine vinavyotambuliwa na Serikali katika mojawapo ya fani zifuatazo: - Maendeleo ya Jamii (Community Development), Sayansi ya Jamii (Sociology), Masomo ya Maendeleo (Development Studies), Mipango na Usimamizi wa Miradi (Project Planning and Management), Jinsia na Maendeleo (Gender and Development), Rural Development.

4.DEREVA DARAJA LA II - (NAFASI 10)

Sifa ya Muombaji Nafasi ya Dereva

Kuajiriwa wenye cheti cha Kidato cha Nne (Form IV) na Leseni ya Daraja E au C ya uendeshaji magari ambayo wamefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja (1) bila kusababisha ajali pamoja na vyeti vya mafunzo vilivyowapatia sifa ya kupata madaraja husika. Wawe wamehudhuria mafunzo ya msingi ya Uendeshaji magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na Chuo cha VETA au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.

Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa:-

MKURUGENZI MTENDAJI (W),

HALMASHAURI YA WILAYA,

S.L.P 126,

BUNDA. 

Maombi yote ya kazi yatumwe kwenye Mfumo wa Kieletroniki wa Ajira (Recruitment  Portal) kupitia anuani ifuatayo: https://portal.go.tz (Anuani hii pia inapatikana  kwenye Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa “Recruitment Portal “).


BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD PDF YA TANGAZO


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Below Post Ad