Nafasi za Mafunzo Kutoka SIDO Tanga
Ofisi yetu imepokea barua yenye Kumb. Na. CA.122/395/06/29 ya tarehe 02.09.2025 yenye kichwa cha habari tajwa hapo juu. Kwa mantiki hiyo inakaribisha maombi kwa vijana wenye uhitaji wa kushiriki mpango wa mafunzo katika Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogo (SIDO – Tanga) kupitia mradi wa Inclu-Cities – SASA.
Mafunzo yatatolewa bure ikiwa ni katika kutekeleza mradi wa "Inclusive Green Smart Cities SASA" unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (European Union) na kutekelezwa kwa ushirikiano wa shirika la maendeleo la Ubelgiji (ENABEL) na SIDO-Tanga kwa lengo la kuwalea na kuwaendeleza vijana na wanawake wajasiriamali katika Jiji la Tanga.
FANI ZITAKAZOTOLEWA MAFUNZO:
1) Usindikaji wa vyakula
2) Utengenezaji wa sabuni na vipodozi
3) Uchomeleaji (uungaji vyuma)
4) Uchakataji wa dagaa
5) Uchakataji wa taka za plastiki
6) Utengenezaji wa mkaa mbadala
SIFA ZA MWOMBAJI:
1. Awe mkazi wa Jiji la Tanga
2. Umri:
• 18–35: Kwa Kijana wa kiume
• 18–60: Kwa wanawake
• 18–60: Kwa watu wenye ulemavu (bila kujali jinsia)
3. Awe anaishi au anafanya shughuli zake katika Jiji la Tanga
4. Awe raia wa Tanzania
5. Awe anajua kusoma na kuandika
6. Awe ameshaanza shughuli za uzalishaji angalau kwa miezi mitatu
7. Awe anajihusisha na moja ya sekta zifuatazo:
• Usindikaji wa vyakula
• Utengenezaji wa sabuni na vipodozi
• Uchomeleaji (uungaji vyuma)
• Uchakataji wa dagaa
• Uchakataji wa taka za plastiki
• Utengenezaji wa mkaa mbadala
8. Awe tayari kushiriki mafunzo/vikao vyote vya SIDO
5. Awe tayari kuwa na mdhamini
6. Awe tayari kusaini hati ya makubaliano