Nafasi za Kazi Mafia Dc 04-09-2025
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri (W) ya Mafia anawatangazia Watanzania wenye sifa kuomba nafasi za kazi mbili (02) katika Halmashauri hii baada ya kupata kibali kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa mchanganuo ufuatao:
1.DEREVA DARAJA LA II – NAFASI 2
Majukumu ya Muombaji
Kuajiriwa wenye cheti cha Kidato cha Nne (Form IV) na Leseni ya Daraja E au C ya uendeshaji magari ambayo wamefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja (1) bila kusababisha ajali pamoja na vyeti vya mafunzo vilivyowapatia sifa ya kupata madaraja husika. Wawe wamehudhuria mafunzo ya msingi ya Uendeshaji magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na Chuo cha VETA au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.
Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa: -
Mkurugenzi Mtendaji,
Halmashauri ya Wilaya ya Mafia,
13 Barabara ya Boma
S.L.P. 85,
61782 MAFIA.