Nafasi Mpya za Kazi Kutoka Buchosa
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Buchosa anatangaza nafasi KUMI NA TANO (15) za kazi ya Mkataba ya wakusanyaji mapato (revenue collectors) ambao wataajiriwa kwa muda wa miezi sita kuanzia Tarehe 1 October hadi Tarehe 31,March 2025 kwa mwaka wa fedha 2025/2026. Mapato hayo yatakusanywa katika vyanzo mbalimbali vya mapato kama vitakavyoonekana kwenye Mikataba itakayoandaliwa baada ya taratibu za ajra ya muda kukalimika.
MAJUKUMU YA KAZI:
1. Kukusanya mapato toka kwenye vyanzo vya mapato atakavyopangiwa
2.Kuhakikisha kuwa makusanyo yote yaliyokusanywa kwa siku hiyo yanawekwa Benki
3. Kuhakikisha kuwa makusanyo yote yanakusanywa kwa kutumia mashine ya kukusanyia mapato (POS MACHINE) na kutoa stakabadhi halali za Halmashauri
4. Kuhakikisha kuwa mashine ya kukusanyia mapato (POS MACHINE) inakuwa katika hali nzuri na inatumika muda wote bila kuzimwa (inakuwa ONLINE)
5. Kuhakikisha kuwa mwajiriwa anatumia Mzani aliopatiwa na Halmashauri kwa ajiri ya kupimia Mizigo (Dagaa,samaki, mchele, mpunga n.k)
6. Kuhakikisha kuwa mteja anapata risiti yake ya mzigo aliolipia kwa wakati pasipo kuchukua pesa mkononi.
7. Kufanya kazi yoyote utakayopangiwa na msimamizi