Majina ya Walioitwa Kazini Jiji la Dar es Salaam
Mkurugenzi wa Halmashaurii ya Jiji la Dar es Salaam anapenda kuwataarifa waombaji kazi wa nafasi za Udereva Daraja la II, Msaidizi wa Kumbukumbu Daraja la II na Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja la II waliofanya usaili kati ya tarehe 14/09/2025 hadi 18/09/2025 matokeo yapo tayari. Waliofaulu usaili huo ni kama yalivyoorodheshwa katika jedwali hili.
Aidha, waombaji kazi waliofaulu usaili wanatakiwa kuripoti kwa mwajiri (Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam) kuanzia tarehe 19/09/2025 hadi tarehe 25/09/2025 baada ya tangazo hili wakiwa na vyeti halisi (Originals Certificates) za masomo kuanzia Kidato cha nne na kuendelea ili vihakikiwe na mwajiri kabla ya kupewa barua ya ajira. Kwa wale ambao majina yao hayapo katika tangazi hili watambue kuwa hawakupata nafasi/hawakufaulu usaili, hivyo wasisite kuomba kwa mara nyingine nafasi za kazi zitakapotangazwa.