WhatsApp Group Join Now

Nafasi Mpya za Kazi at Musoma Dc 2025

 

Nafasi Mpya za Kazi at Musoma Dc 2025

Sekretarieti ya Ajira Portal kupitia ajira.go.tz imetangaza nafasi za kazi kwa wataalamu wa Msaidizi wa Kumbukumbu, Dereva daraja la pili pamoja na mwendesha ofisi. Jumla ya Nafasi hizo 14 at Musoma Dc waombaji wote wenye sifa (qualications) wanaombwa kutuma maombi ya kupitia portal.ajira.go.tz kabla ya tarehe 12 septemba 2025. Zifuatazo ni baadhi ya nafasi na majukumu yake:

1.MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA II

Majukumu ya Kazi

1. Kuorodhesha barua zinazoingia Masjala kwenye regista ya barua zinazoingia (incoming correspondence register).

2. Kuorodhesha barua zinazotoka nje ya taasisi kwenye regista ya barua zinazotoka (outgoing correspondence register).

3. Kusambaza majalada kwa Watendaji (action officers).

4. Kupokea majalada kutoka kwa Watendaji (action officers).

5. Kupokea majalada yanayorudi Masjala toka kwa Watendaji.

6. Kurudisha majalada kwenye shabaka/kabati la majalada (racks/filling cabinets) au sehemu nyingine yanapohifadhiwa.

7. Kufuatilia mzunguko wa majalada ndani ya Taasisi (file tracking).


READ MORE AND APPLY JOB HERE

2. DEREVA DARAJA II

Duties and Responsibilities

1. Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari.

2. Kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi.

3. Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari.

4. Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali.

5. Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari.

6. Kufanya usafi wa gari.

7. Kufanya kazi nyingine kadri atakavyoelekezwa na Msimamizi wake.


READ MORE AND APPLY JOB HERE

3. MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA II

Duties and Responsibilities

1. Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida na za siri.

2. Kupokea wageni, kusikiliza shida zao na kuwaeleza wanapoweza kusaidiwa.

3. Kutunza taarifa za kumbukumbu ya matukio, miadi, tarehe za vikao, safari za Mkuu wake na ratiba za kazi zingine.

4. Kutafuta majalada na nyaraka zinazohitajika katika utekelezaji wa majukumu ya kazi.

5. Kupokea majalada na kusambaza kwa Maofisa walioko katika Idara/Kitengo/Sehemu husika.

6. Kukusanya, kutunza na kurejesha majalada na nyaraka sehemu zinazohusika.

7. Kupanga dondoo na kufanya maandalizi ya vikao mbalimbali.

8. Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya ofisi.

9. Kufanya kazi zingine atakazopangiwa na Mkuu wake wa kazi.


READ MORE AND APPLY JOB HERE


DOWNLOAD PDF HERE


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Below Post Ad