Majina ya Waombaji Waliochaguliwa Chuo Zaidi ya Kimoja (Multiple Admission) 2025/2026 First Round
Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kinapenda kuwafahamisha waombaji wote waliopata udahili katika vyuo/programu zaidi ya moja kwa mwaka wa masomo 2025/2026 kwamba, ili kujiunga rasmi na programu ya masomo UDOM, ni lazima mwombaji husika athibitishe udahili wake.
Uthibitisho wa udahili lazima ufanyike kuanzia tarehe 3 Septemba 2025 hadi tarehe 21 Septemba 2025.
Hatua za kuthibitisha udahili:
1. Ingia kwenye akaunti yako ya udahili kupitia mfumo wa udahili wa UDOM: https://application.udom.ac.tz
2. Omba namba maalum ya uthibitisho kupitia kiungo kilichopo kwenye akaunti yako ya udahili.
3. Utapokea namba maalum (SPECIAL CODE) kupitia SMS au barua pepe.
4. Weka namba hiyo maalum kwenye akaunti yako ya udahili ili kukamilisha uthibitisho.
DOWNLOAD UDOM MULTIPLE SELECTION ATTACHEMEN HERE
PDF OF MULTIPLE ADMISSIONS FROM TCU