Ajira Mpya 1200 za Afya na Elimu Endapo Dkt. Samia Ataendelea Kupewa Ridhaa
Mgombea wa Urais kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameahidi kuwa endapo ataendelea kupewa ridhaa ya kuongoza nchi katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 29, 2025, Serikali yake ndani ya siku 100 itaajiri watumishi wapya 5,000 wa kada ya Afya na 7,000 wa kada ya Elimu.
Dkt. Samia alitoa kauli hiyo Septemba 11, 2025, katika mkutano wa kampeni uliofanyika Viwanja vya Tarafa ya Uyui, Kata ya Ilolanguru, wilayani Uyui, mkoani Tabora. Katika hotuba yake, alieleza kuwa ajira hizo zitalenga kuboresha ustawi wa sekta ya Afya na Elimu, pamoja na kuzalisha fursa zaidi za ajira kwa Watanzania.
Umuhimu wa Ajira Hizi
Ajira za kada ya Afya zitasaidia kupunguza changamoto ya upungufu wa wahudumu katika hospitali, vituo vya afya na zahanati nchini. Hii itaboresha upatikanaji wa huduma bora za afya, hasa kwa wananchi wa maeneo ya vijijini.
Kwa upande mwingine, ajira za kada ya Elimu zitaleta walimu wapya 7,000 ambao watasaidia kupunguza tatizo la upungufu wa walimu mashuleni. Hatua hii inalenga kuongeza kiwango cha ufaulu na kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia.