Nafasi za Kazi za Mkataba Walimu wa Secondary 2025 Tunduru Dc
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri a Wilaya ya Tunduru anapenda kuwatangazia watanzania wote wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi za kazi za Mkataba a Mwalimu Ill , K w a Masomo ya Biashara(Nafasi 31),Kiingereza(Nafasi 02) na Historia( Nafasi 02).Hivyo anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa za kujaza nafasi hizo;-
Masharti ya Jumla kwa Waombaji wa Kazi
Waombaji wote wa nafasi za kazi wanatakiwa kuzingatia masharti yafuatayo kabla ya kuwasilisha maombi yao:
1. Uraia na Umri
- Mwombaji lazima awe Raia wa Tanzania.
- Awe na umri kuanzia miaka 18 hadi 45.
2. Waombaji Wenye Ulemavu
- Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi.
- Wanaombwa kuainisha aina ya ulemavu wao kwenye mfumo wa kuombea ajira kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
3. Wasifu wa Mwombaji (Detailed C.V)
Kila mwombaji anatakiwa kuambatanisha:
- Maelezo binafsi ya kina (Curriculum Vitae - C.V).
- Anuani halisi inayotumika.
- Namba za simu zinazopatikana muda wote.
- Anuani ya barua pepe (Email Address).
- Majina ya wadhamini watatu (Referees) wa kuaminika.
4. Vyeti vya Elimu na Taaluma
Maombi yote lazima yaambatane na nakala zilizothibitishwa kisheria za vyeti vya kielimu na kitaaluma kulingana na kiwango cha elimu:
- Cheti cha Kidato cha Nne (Form Four Certificate).
- Cheti cha Kidato cha Sita (Form Six Certificate).
- Vyeti vya Mafunzo ya Juu kama: Postgraduate, Degree, Advanced Diploma, Diploma au Certificate.
- Computer Certificate.
- Vyeti vya Kitaaluma (Professional Certificates) kutoka bodi husika.
- TCU – Tanzania Commission for Universities.
- NECTA – National Examinations Council of Tanzania.
- NACTVET – National Council for Technical and Vocational Education and Training.