Matokeo ya Darasa la Saba 2024 (NECTA PSLE) Yatangazwa Rasmi
Dar es Salaam, Oktoba 29, 2024 – Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limetangaza rasmi matokeo ya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi (PSLE) 2024, uliofanyika Septemba 2024 katika maeneo yote ya Tanzania Bara na Zanzibar.
Akitangaza matokeo hayo, Katibu Mtendaji wa NECTA, Dkt. Said Mohamed, alisema jumla ya watahiniwa 1,230,774 walisajiliwa kufanya mtihani huo. Kati yao:
1. Wasichana: 666,597 (sawa na 54.16%)
2. Wavulana: 564,177 (sawa na 45.84%)
Kwa upande wa wanafunzi wenye mahitaji maalum, jumla ya 4,583 sawa na 0.37% ya wote waliosajiliwa walihusishwa na mtihani huo.
Kati ya watahiniwa wote waliokuwa wamesajiliwa, 1,204,899 (sawa na 97.90%) waliweza kufanya mtihani. Hii ilijumuisha:
1. Wasichana: 656,160 (98.43%)
2. Wavulana: 548,739 (97.26%)
Hatua za Kuangalia Matokeo ya Darasa la Saba (NECTA – PSLE)
Kama unataka kutazama matokeo ya Darasa la Saba - PSLE, nenda google kisha search neno NECTA. Matokeo ya google yataonesha website mbalimbali, chagua website rasmi ya NECTA kisha fuata hatua zifuatazo:
1. Tembelea tovuti rasmi ya NECTA:
2. Fungua NECTA website na nenda kwenye sehemu ya “Results” (Matokeo) .
3. Chagua PSLE kama aina ya mtihani unayotaka kuangalia.
4. Chagua mwaka husika ( mfano, 2024 au 2023) .
5. Kisha chagua mkoa, wilaya/district, na shule ulipoendelea.
MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024